Wabunge wa muungano wa Azimio wapinga vikali ubinafsishaji wa mashirika ya umma

  • | K24 Video
    206 views

    Wabunge wa muungano wa Azimio wamepinga vikali hatua ya baraza la mawaziri kuidhinisha mswada wa kubinafsisha mashirika ya serikali bila idhini ya bunge. Muungano huo unadai kuna njama ya kunyakua mali ya umma na ardhi kupitia hatua ya baraza la mawaziri. Qanasema bandari ya Mombasa, taasisi ya uchunguzi na matibabu ,KEMRI, kampuni za sukari pamoja na vyuo vikuu vya Egerton na Kenyatta ni baadhi ya mashirika ya umma yanayopangiwa kuuzwa. Viongozi wa seneti aidha wanashikilia kuwa mswada huo hauna uhalali kwani mabadiliko yanayohusisha bunge yanapaswa kufanyika kupitia kura ya maoni.