Wafanyakazi wa kampuni ya maji ya Malindi waandamana kulalamikia usimamizi mbaya kwenye kampuni hiyo

  • | Citizen TV
    124 views

    Shughuli za kawaida zimetatizika kwa muda katika ofisi za kampuni ya usambazaji maji ya Malindi baada ya wafanyikazi wa kampuni hiyo kuandamana kwa madai ya kunyanyaswa na usimamizi wa kampuni hiyo. Polisi walilazimika kutumia vitoa machozi kuwafurusha waandamanaji hao huku wengine kujeruhiwa katika rabsha hiyo. Wafanyikazi hao wanadai kuwa wamekuwa wakikatwa pesa katika mishahara yao kwa ajili ya hazina mbali mbali huku hela hizo zikikosa kupelekwa zinakohitajika. Waziri wa maji katika serikali ya Kilifi Omar Said amewahakikishia wafanyikazi hao kuwa serikali ya Kilifi itazingatia kilio chao kwa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu madai yao ili kutoa suluhu.