Wafuasi wa Azimio watakiwa kufanya dua za waathiriwa wa maandamano

  • | Citizen TV
    2,090 views

    Muungano wa Azimio ulisitisha maandamano ya leo na badala yake kuwaagiza wafuasi wake kuwakumbuka waliouwawa pamoja na waliojeruhiwa kwenye maandamano kwa njia ya maombi na kukesha wakiwasha mishumaa. Viongozi wa muungano huo wamepanga kutembelea waathiriwa katika hospitali kadhaa hapa jijini Nairobi ikiwemo ya Mama Lucy. kwa sasa wanazungumza na wanahabari kabla ya kuanza shughuli za leo. tusikilize wanayosema