Wahudumu wa afya wapuuzilia mbali vitisho vya serikali

  • | Citizen TV
    1,901 views

    Wahudumu wa afya wanaogoma wameshikilia kuwa kamwe hawatatishwa kusitisha mgomo wao licha ya vitisho kutoka kwa asasi za kiusalama. Maafisa wa miungano ya madaktari, maafisa kliniki na ule wa wahudumu wa maabara wamesema kuwa hawatarejea kazini hadi matakwa yao yasikilizwe. Kwa upande mwingine, mkuu wa utumishi wa umma felix koskei amepuuzilia mbali mkataba unaolumbaniwa uliotiwa saini na serikali mwaka wa 2017.