Wahudumu wa matatu walalamikia ongezeko la ajali Ilbissil katika kaunti ya Kajiado

  • | Citizen TV
    287 views

    Wahudumu kwenye sekta ya uchukuzi mjini Ilbissil kaunti ya Kajiado wanalalamikia kuongezeka kwa ajali zinazosababishwa na malori ya masafa marefu huku hatua dhidi ya wahusika ikikosa kuchukuliwa. Wahudumu hao walizuia lori lililosabisha ajali katika barabara ya Namanga wakilalamikia kisa cha hivi punde zaidi ambapo mmoja wao aligongwa na lori lilikokuwa likiendeshwa kwa kasina kufariki. Wanadai mmiliki wa lori hilo alikuwa anapanga kuondoa lori lake katika kituo cha polisi, wakihofia kuwa uhenda haki ikakosa kutendeka. Wanaitaka idara za usalama hasa katika barabara kuu ya Namanga kuwajibika wakidai kuwa tangu mwaka wa 2021 zaidi ya watu 20 wakiwemo madereva wanaoendesha matatu wamefariki huku haki ikikosa kupatikana.