Wakazi Mombasa bado wana wasiwasi wa kimbunga Hidaya

  • | KBC Video
    48 views

    Licha ya tangazo la idara ya utabiri wa hali ya anga kwamba hakuna tishio la kimbunga Hidaya kukumba pwani ya Kenya na kuthibitisha kwamba kilikumba pwani ya Tanzania, shughuli za kawaida kwenye fuo nyingi jijini Mombasa bado hazijarejelewa. Uchunguzi uliofanywa na runinga ya KBC channel 1 kwenye ufuo wa umma wa Jomo Kenyatta jijini Mombasa ulionyesha maafisa wa polisi wakishika doria kwenye fuo na kuwazuia umma kuingia humo licha ya marufuku dhidi ya shughuli za fuoni yaliyowekwa na waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki kufikia kikomo usiku wa manane. Wafanyabiashara wanaotekeleza shughuli zao kwenye ufuo huo pia hawawezi kutekeleza shughuli zao. Wanalalamikia kuendelea kukosa mapato hali ambayo wanasema itaathiri vibaya biashara zao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive