Wananchi waraiwa kusaidia familia zinazoathirika na njaa

  • | Citizen TV
    184 views

    Huku watu zaidi ya milioni nne nukta tano wakikumbwa na baa la njaa nchini, wito umeendelea kutolewa kwa wakenya kujiunga ili kusaidia familia hizo haswa wakati huu wa krismasi. Kulingana na kamati inayoangazia ukame na njaa nchini, bilioni 57 zinahitajika ili kukabiliana na hali hiyo ambayo imeathiri kaunti zaidi ya 30. Wakenya wametakiwa kulinda misitu na kuzingatia upanzi wa miti kama njia moja ya kukabiliana na kiangazi.