Watu 93 wamefariki kutokana na mafuriko kufikia sasa

  • | Citizen TV
    3,985 views

    Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko nchini imeongezeka kufikia 93 hii leo, baada ya watu 10 zaidi kufariki kaunti za Garissa na Homa Bay. Vifo hivi vimejiri huku maelfu wakiathirika na mifugo zaidi wakisombwa kutokana na athari za mvua kubwa inayoendelea kunyesha sehemu nyingi nchini. Na kama Brenda Wanga anavyotuarifu, mvua hizi zimeendelea kuathiri maisha ya wengi na kuzidi kusababisha maafa