Waziri Kithure Kindiki aagiza timbo na migodi isiyo salama katiak kaunti ya Busia kufungwa

  • | Citizen TV
    279 views

    Waziri wa usalama wa kitaifa Prof. Kithure Kindiki ameagiza msako wa matimbo yoye yanayochimbwa madini na kufungwa kwa yale yasiyoafiki viwango na kuwa hatari kwa maisha ya wachimbaji. Akizungumza katika timbo la uchimbaji dhahabu la Bumutiru, eneo bunge la Butula, kaunti ya Busia, Kindiki amesisitiza kuwa lengo kuu la serikali ni kuchukua hatua za kiusalama kuzuia mikasa kuliko pilka pilka za uokoaji baada ya majanga.