Waziri Linturi adai mpenziwe wa zamani amedhamini hoja ya kumtimua

  • | Citizen TV
    3,786 views

    Waziri wa Kilimo Mithika Linturi ambaye amekana kuhusika na kashfa ya mbolea ghushi, amedai mpenziwe wa zamani ambaye ni mbunge wa Aldai ndiye mdhamini wa hoja ya kumuondoa mamlakani Kama waziri. Hatahivyo, mlalamishi mkuu kwenye kesi hiyo mbunge wa Bumula Jack Wamboka, amekana madai hayo na kuielezea kamati inayomchunguza Linturi kwamba anatetea maslahi ya wakulima kote nchini na wala sio kwa niaba ya mdhamini yeyote.