Zaidi ya nyumba 1,200 zimesombwa na maji Isiolo

  • | Citizen TV
    2,477 views

    zaidi ya nyumba 1,200 katika eneo la Merti kaunti ya Isiolo wamelazimika kuhama kwao kufuatia mafuriko. Hii ni baada ya mto Ewaso Nyiro kuvunja kingo zake na maji kuzingiramji wa Merti. takriban shule saba zimeathirika na mafuriko huku misikiti minne pia ikijaa maji. usafiri wa watu na uchukuzi wa mizigo umetatizika huku barabara zinazotumiwa kusafirisha bidhaa na chakula zikiharibiwa na mafuriko na kusababisha magari kukwama kati ya eneo la Bulesa na Merti. wakazi wanahofia kuwa hali hiyo itasababisha uhaba wa chakula. aidha kuna hofu ya mlipuko w amaradhi kutokana na vyoo kusombw ana maji. gavana wa kaunti ya isiolo Abdi Ibrahim Guyo ambaye alizuru maeneo yaliyoathirika amewataka wakazi kuchukua tahadhari wakati huu ambapo mvua kubwa inazidi kunyesha.