Chama cha matabibu nchini Kenya kimetishia kuanza mgomo kote nchini kuanzia saa sita usiku kutokana na kutotekelezwa kwa ahadi za Wizara ya Afya na baraza la Magavana. Chama hicho kinadai kucheleweshwa kutiwa saini mkataba wa makubaliano ya pamoja ulioidhinishwa wa mwaka 2024, kuajiriwa kwa wahudumu wa Afya kwa Wote kwa masharti ya kudumu,yakiwemo malimbikizi ya malipo ya mishahara kwa wafanyikazi wa hazina ya kimataifa. Chama hicho kimeishutumu Wizara ya Afya kwa ulegevu na ukosefu wa nia njema, wakiapa kutofanya kazi hadi matakwa yao yote yatimizwe.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive