- 634 viewsDuration: 3:03Huku wanafunzi wa gredi ya kumi wakiendelea kuripoti shuleni, ndoto za mamia ya wanafunzi wengine wanaotoka familia zisizojiweza zimesalia njiapanda. Katika mtaa wa Mukuru kwa Njenga hapa Nairobi, kijana Nicholas Otieno amelazimika kufanya kazi ya kusukuma mikokoteni kuuza maji angalau kuchangisha karo yake. Ni hali sawa na ya binti mmoja Ruth Akiru huko Trans Nzoia ambaye sasa amekosa matumaini ya kuendelea na masomo.