Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa kidini huko Kuria wanalalamikia kuvamiwa

  • | Citizen TV
    282 views
    Duration: 1:52
    Viongozi wa kidini kutoka Maeneo ya Kuria ambao wamekuwa wakipambana na ukeketaji wa mtoto msichana wanakabiliwa na uhasama kutoka kwa wananchi ambao bado wamekumbatia Mila hiyo potovu. Wakiongozwa na kiongozi wa kanisa la kiadventista tawi la Kuria Paul Girimbe, baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa wakizungumza waziwazi kuhusu masuala ya ukeketaji wameshashambuliwa na kujeruhiwa huku akiongeza kuwa wengine bado wanalengwa. Girimbe alisema wanahitaji uchunguzi wa kina ufanywe na polisi ili waathiriwa wapate haki. Mbali na uadui dhidi ya viongozi wa dini, Girimbe amesema wanaume waliopitia tohara ya kimatibabu pia wanalengwa, akiongeza kuwa baadhi yao wamelazimishwa kupitia tohara ya kitamaduni.