- 193 viewsDuration: 1:18Madaktari katika hospitali za umma kaunti ya Nairobi wameapa kutositisha mgomo wao hadi pale kaunti itakapolipa mishahara yao yote na marupurupu. Madakatari hao ambao wamekua wakishiriki mgomo huo tangu desemba 18 wameikashifu serikali ya gavana johnson sakaja kwa kukosa kulipa mishahara pamoja na marupurupu yao, huku wakisema kwamba kaunti ya nairobi inazidi kupuuza makubaliano yao. Haya yanajiri wakati maafisa tabibu nao wakiwa kwenye mgomo wa siku ishirini na moja sasa.