Skip to main content
Skip to main content

Mzozo wa ardhi Sabaki

  • | Citizen TV
    174 views
    Duration: 2:10
    Mzozo umezuka upya baina ya wakaazi wa Sabaki na usimamizi wa ardhi ya ADC kisiwani mjini Malindi kufuatia kile wakaazi wa eneo hilo wanachodai kama kuhangaishwa na usimamizi wa ADC eneo hilo. Katika taarifa yake kwa kituo cha eneo hilo, mwakilishi wadi wa Sabaki Rose Baraka amelalamikia vikali kukamatwa kiholela kwa wakaazi wa eneo hilo wanapozuru shamba hilo. Kiongozi huyo ameteta kuhusu kutiwa nguvuni ovyo ovyo kwa wakaazi wa eneo hilo na kuitaka serikali kukomesha mara moja mzozo huo. Kauli yake imepigwa jeki na kiongozi wa vijana eneo hilo Johnathan Ngala ambaye amesisitiza haja ya ardhi hiyo kugawanyiwa wakaazi kwa misingi kuwa ADC haina tena mamlaka juu yake.