- 1,743 viewsDuration: 1:31Raia wawili wa uturuki ambao ni wakimbizi na wafanyabiashara wataendelea kuzuiliwa kwa siku 14 ili kutoa fursa kwa maafisa wa polisi kitengo cha ugaidi kukamilisha uchunguzi. Wawili hao wanaokabiliwa na tuhuma za kufadhili ugaidi walikamatwa na kufikishwa katika mahakama ya mombasa. Upande wa mashtaka ulitaka siku 21 ili kukamilisha uchunguzi. Mawakili wa washukiwa wamelalamikia kuzuiliwa kwa wawili hao wakidai hakuna ushahidi uliopatikana kabla ya kukamatwa kwao wakidai kesi hiyo ilibadilishwa kwa madai ya shambulio la ajali hadi ugaidi.