Wanafunzi wa Shule ya Umma ya Senior Chief Mutunkei iliyoko Kajiado Mashariki, pamoja na wakazi wa eneo hilo, wamepata tabasamu baada ya kuchimbiwa kisima cha maji na shirika lisilo la serikali. Mradi huo, uliozinduliwa na Gavana wa Kaunti ya Kajiado, Joseph Ole Lenku, unalenga kufaidi zaidi ya wanafunzi 400 katika shule hiyo.
Lengo kuu la mradi huo ni kuimarisha uzalishaji wa chakula shuleni na kupunguza makali ya njaa, hususan katika kaunti ya Kajiado ambayo imekuwa ikikumbwa na changamoto ya ukame wa mara kwa mara.