- 105 viewsDuration: 1:07Baadhi ya wakazi katika kaunti ya bungoma wameipa serikali makataa ya siku tatu kuhakikisha ofisi ya masoroveya mjini humo imefunguliwa mara moja ili kutoa huduma kwa umma. Wakizungumza baada ya maandamano ya kupinga uhamisho wa afisa mkuu wa masoroveya mjini humo,wakaazi hao wanadai uhamisho huo umesitisha huduma muhimu za usoroveya kwa kuwa afisa aliyeletwa kutokea kaunti ya busia hajakubalika kutokana na madai ya ufisadi dhidi yake.