Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi 3 wa gredi ya 10 warudia gredi ya 9 kwa kukosa karo

  • | Citizen TV
    1,492 views
    Duration: 1:34
    Wanafunzi watatu waliokamilisha masomo yao ya gredi ya Tisa katika shule ya msingi ya Mupeli mjini Bungoma na kuitwa kujiunga na shule za C1 za gredi ya kumi wamelazimika kurudia gredi ya Tisa kutokana na ukosefu wa karo . Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Everlyne Wambaya, walishangazwa kuwaona wanafunzi hao wakirejea shuleni na kuingia gredi ya Tisa ilhali walikuwa wamefuzu vyema kujiunga na gredi ya kumi. Wanafunzi hao shannel Wakoli, Emelisa Sheroya na Fayzeen Simiyu waliopata alama za 59,64 na 62 mtawalia wanasema kuwa huenda ndoto zao zikadidimia kutokana na ukosefu wa karo.