- 396 viewsDuration: 1:50Mwanasheria mkuu Dorcas Oduor anasema ofisi yake imeanza mchakato wa kupiga darubini sheria zilizopo kukabiliana na uuzaji na usambaji wa dawa za kulevya. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ofisi za kutoa mafunzo kuhusiana na sheria katika ofisi yake, mwanasheria mkuu amesema wataweka sheria kali za kukabiliana na biashara hiyo haramu ikiwemo serikali kuchukua mali ya wale wanaohusika kuwaangamiza vijana. Oduor anasema kumekuwa na changamoto ya kukabili hali hii kisheria na kwamba idara yake inafanya kila jitihada kuhakikisha sheria mpya itasaidia kukabili hali mara moja.