- 253 viewsDuration: 1:18Maafisa wa mamlaka ya ukusanyaji ushuri nchini KRA wamenasa shehena bandia ya sigara katika bandari ya Mombasa ambazo zilipangiwa kuingia kwenye soko la humu nchini. Kulingana na kra sigara zaidi ya milioni 9.3 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 281 zinazuiliwa katika kituo cha polisi cha kilindini baada ya kufanyiwa ukaguzi kwa ushirikiano na vitengo husika na kubainika kuwa shehena hiyo ilikuwa imetoka singapore na kuingia nchini. Kulingana na stakabadhi tulizoziona, mmiliki wa shehena hiyo alidai kuwa kontaina hiyo ilikuwa imetoka sudan ilihali ilikuwa imetoka cambodia ikipitia singapore kisha kuingia nchini.maafisa wa kra wanadai ni njama ya wafanyabiasha kukwepa kulipa ushuru wa shilingi milioni 83.