- 2,047 viewsDuration: 2:01Mwanafunzi mmoja Shadrack Kipngeno kutoka shule ya msingi ya Itembe katika kaunti ya Bomet aliamka na kutembea kwa miguu kilomita sitini hadi katika shule ya upili ya Kabartegan kaunti ya Kericho bila chochote ila barua ya mwaliko pekekee. Mwalimu mkuu wa shule hiyo Kiprono Chelule alimpokea kijana huyo na kumnunulia vifaa vya mahitaji yake yote kisha kulipia karo baada ya kuona ari yake ya masomo na kwamba anatoka katika familia masikini.