- 274 viewsDuration: 1:30Idara ya afya imetakiwa kuanzisha mchakato wa kutoa hamasisho kwa umma kuhusu umuhimu wa kufanya ukaguzi wa saratani ya kizazi mapema iwezekanavyo. Kulingana na madaktari wa saratani hapa nairobi, idadi kubwa ya wagonjwa nchini hufika hospitalini kwa matibabu baada ya kuathirika kwa muda mrefu kutokana na ukosefu wa ufahamu wa saratani ya kizazi. Wanaoathirika zaidi na jinamizi hili ni akina mama wanao ishi mashambani kutokana na kile kimetajwa kuwa kukithiri kwa umaskini na mila potovu.