Viongozi kutoka eneo la Rabai katika kaunti ya Kilifi wametoa wito kwa kampuni zinazoendeleza shughuli zao katika eneo hilo kuwa kwenye mstari wa mbele kutekeleza miradi ya kijamii. Wakiongozwa na naibu gavana wa Kilifi Florah Chibule, viongozi hao walisema kuwa kando na kutoa fursa za kazi ,kampuni hizo zina jukumu la kuboresha maisha ya wakazi kwa kutekeleza miradi itakayowanufaisha moja kwa moja . Chibule alizungumza wakati wa kufungua rasmi zahanati iliyojengwa na kampuni ya kawi ya Rabai Power.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive