Wavuvi katika kaunti ya Kwale wamepinga zoezi linaloendeshwa na kamati ya bunge la kitaifa ya uchumi wa baharini la kukusanya maoni ya mswada wa usimamizi na maendeleo ya uvuvi wa 2023 wakisema muda uliowekwa ni mchache.Wakizungumza huko Tiwi wakati wa kikao cha kukusanya maoni kuhusu mwada huo, wavuvi hao wameshikilia kuwa wavuvi wengi wanaokumbana na changamoto baharini hawajapata nafasi ya kushirikishwa kikamilifu ili kujumuisha maoni yao kwenye mswada huo. Hata hivyo, mwenyekiti wa kamati hiyo Kangogo Bowen ameitaka wizara ya ardhi kutatua mizozo iliyopo ya unyakuzi wa sehemu zilizotengewa bandari za uvuvi wa samaki eneo hilo.