- 320 viewsDuration: 1:14Serikali ya Kaunti ya Lamu, kwa kushirikiana na Shirika la WWF, imejenga bwawa la maji katika eneo la Pangani litakalotumiwa na jamii ya wafugaji kunywesha mifugo wao ili kupunguza migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Migogoro hiyo imeendelea kushuhudiwa katika eneo la Pangani kutokana na wakulima kuvamia chemichemi za maji ya wafugaji na kusababisha wafugaji kukosa sehemu ya malisho.