- 3,733 viewsDuration: 3:19Jaji mkuu mstaafu David Maraga alikuwa miongoni mwa wanaharakati 9 waliokamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Lang’ata siku ya jumatatu kabla ya kuachiliwa baadaye. Tisa hao walikuwa kwenye maandamano ya kupinga kuhamishwa kwa mbuga ya wanyama ya Nairobi na ujenzi wa eneo la maegesho ya magari kwenye ekari 89 ya ardhi ya mbuga ya kitaifa ya wanyama. Hata hiyo shirika la KWS latetea mradi huo.