Shughuli za kibiashara zimeanza kurejea katika eneo la South C, siku kumi baada ya jengo kuporomoka na kusababisha vifo vya watu wawili.
Wafanyabiashara sasa wanajitahidi kurejesha hali ya kawaida huku wakikabiliana na athari za mkasa huo. Ingawa baadhi ya maduka tayari yamefunguliwa tena, mengine bado yamesalia kufungwa, huku wamiliki wakisema tukio hilo liliathiri pakubwa shughuli zao. Wakati wa zoezi la kusafisha, wafanyabiashara wanaofanya kazi karibu na jengo lililoporomoka walisema walipata hasara kubwa kutokana na wizi na uharibifu wa mali