Serikali imetoa wito kwa sekta ya kibinafsi kuunga mkono juhudi za kuwawezesha wanawake humu nchini. Mshauri wa afisi ya rais kuhusu haki za wanawake, Harriette Chaggai, amesema tangu mwaka-2022, utawala wa Kenya Kwanza umedhihirisha kujitolea kwake kuhakikisha wanawake zaidi wameteuliwa katika nyadhifa za uongozi nchini. Chiggai, hata hivyo amesema hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha kwamba sera kama vile kanuni ya uakilishi sawa wa kijinsia, zimeafikiwa hapa nchini.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News