- 16,204 viewsDuration: 3:11Mzozo umeendelea leo kuhusu upeperushaji wa moja kwa moja wa matokeo ya uchaguzi, kufuatia ripoti kuwa Bunge lilifanyia marekebisho Mswada wa Uchaguzi wa mwaka 2024. Baadhi ya viongozi wa upinzani pamoja na Chama cha Wanasheria wamekosoa ripoti hiyo. Hata hivyo, kama Emmanuel Too anavyoripoti, Bunge la Kitaifa limepuuzilia mbali madai hayo, likisema kipengele hicho bado kipo katika sheria na kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao yatapeperushwa moja kwa moja kama ilivyo desturi.