- 1,136 viewsDuration: 2:40Maswali yanaibuka kuhusu ni nani alishindwa kutekeleza majukumu yake kufuatia kifo cha Amos Isoka aliyeaga dunia baada ya kung'olewa jino na daktari bandia mtaani Kawangware. Chama cha Madaktari wa Meno kimeshutumu tukio hilo na kunyoshea kidole cha lawama Baraza la madaktari KMPDC ,ambalo lina jukumu la kuwatambua madaktari bandia. Baada ya siku 16, hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka kwa serikali kuhusu kifo cha Isoka au hata kukamatwa kwa mshukiwa