Kile kilichoanza kama jitihada za familia za kumzika mwanao kwa heshima kimechukua mkondo wa kusitikisha huko Rongo, kaunti ya Migori. Baada ya mapambano mahakamani, makabiliano na maswali ambayo hayajajibiwa maafisa wa polisi wanaotekeleza agizo la mahakama walifukua kaburi lililoaminika kuwa na mwili wa afisa wa kitengo cha GSU, Dan Ayoo. Badala yake maafisa wa polisi walipata mwili tofauti na hivyo kuibua maswali zaidi kuhusu jinsi alivyozikwa kwenye uwanja wa kanisa katika kaunti ya Migori ambako inashukiwa kwamba afisa huyo alizikwa kwa siri mwaka uliopita. Mwanahabari wetu Ben Chumba anatuarifu zaidi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive