Skip to main content
Skip to main content

Familia moja Namanga yamtafuta mpendwa wao

  • | Citizen TV
    404 views
    Duration: 2:02
    Familia moja mjini Namanga, Kaunti ya Kajiado, inaendelea kuishi katika huzuni baada ya ndugu yao kutoweka nchini Afrika Kusini miaka tisa iliyopita. Silas Kipkorir Butia alisafiri hadi Johannesburg mwaka 2017 kutafuta kazi ya udereva wa malori, lakini mawasiliano yake na familia yalikoma ghafla miezi sita baadaye. Licha ya juhudi za kumtafuta, ikiwemo kuwasiliana na ubalozi wa Kenya, familia hiyo bado haijapata majibu kuhusu alipo. Sasa mkewe pamoja na watoto wao watatu wanaishi kwa jamaa huku wakikabiliwa na changamoto za maisha, wakisubiri kwa matumaini kupata ukweli kuhusu hatima yake.