Gavana wa kaunti ya Mandera Mohamed Adan Khalif, amepuuzilia mbali madai ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, kwamba amejenga nyumba katika ardhi inayomilikiwa na shule katika eneo la Parklands, Nairobi, akisema kuwa madai hayo ni ya uongo na yamechochewa kisiasa. Gachagua alimshtumu gavana huyo wakati wa mahojiano, ambapo alimtuhumu kwa kunyakua ardhi ya umma, kwa maslahi ya kibinafsi. Matamshi ya Gachagua yameibua hisia hasa kutoka kwa viongozi na wataalamu kutoka eneo la Kaskazini mwa nchi hii, huku baadhi ya vyombo vya habari vikisusia mahojiano kutokana na madai ambayo hayajadhibitishwa na mgawanyiko. Katika taarifa yake gavana Khalif, amesema ardhi hiyo aliipata kwa njia halali mwaka 2020, kabla ya kuwa gavana wa kaunti ya Mandera . Pia amesema kwamba suala hilo lipo mahakamani na linapaswa kutatuliwa kisheria badala ya shutma kupitia vyombo vya habari. Aidha gavana huyo amesema amewaagiza mawakili wake kumchukulia hatua za kisheria Gachagua kwa kumharibia sifa .
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive