- 982 viewsDuration: 1:31Gavana wa Nyamira Amos Nyaribo anasubiri kujua hatma yake baada ya siku nzima ya majibizao kati ya maseneta na mawakili wake kubaini iwapo mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake yalikuwa na uzito wa kumfanya atimuliwe au la. Mawakili wake waliteta kuwa idadi ya waliotajwa kuidhinisha kubaduliwa kwake haikuwa ya kweli kwani kulikuwa na wawakilishi wadi 19 pekee ilhali rekodi za bunge la kaunti zinaonyesha kuwa wawakilishi wadi 23 walipitisha kubanduliwa kwake. aidha Nyaribo alikana mashtaka yote na kuwataka maseneta kutupilia mbali hoja ya kumbadua ofisini.