Hospitali ya kitaifa ya Kenyatta na muungano wa kitaifa wa wauguzi na wakunga nchini wameafikia mkataba mpya wa maelewano unaobainisha masharti ya ajira, mishahara na kupandishwa vyeo kwa wataalamu walioajiriwa kwa masharti ya kudumu na wale wa kandarasi. Kuambatana na mkataba huo uliotiwa saini leo kwa kipindi cha miaka 2025 hadi 2029, wauguzi na wakunga watapata marupurupu mbalimbali yakiwemo yale ya sare, huduma za uuguzi na mfumo mahsusi wa wauguzi walioajiriwa kwa kandarasi kuajiriwa kwa masharti ya kudumu kuanzia tarehe mosi mwezi Julai mwaka huu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive