- 4,079 viewsDuration: 1:56Msaidizi wa inspekta Jenerali wa polisi Lazarus Opicho atazikwa siku ya Ijumaa nyumbani kwake Kitale, kaunti ya Trans Nzoia. Wakati wa ibada ya wafu iliyowaleta pamoja jamaa, marafiki na wafanyakazi wenza katika kanisa la Friends Church lililoko Lang’ata katika kaunti ya Nairobi, Opicho alitambuliwa kuwa kiongozi mwenye upendo, aliyejali pamoja na mwenye jitihada katika kazi yake. Opicho aliaga dunia tarehe 28 mwezi Septemba mwaka huu wakati alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive