- 637 viewsDuration: 1:52Baraza la kitaifa kuhusu utekelezaji wa haki limeanza kujianda kwa uchaguzi mkuu ujao likisema kamati zote zitaanza kupokea mafunzo ili kujiandaa kikamilifu kwa uchaguzi huru na wa haki. Jaji mkuu Martha Koome ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo ametaka taasisi husika kufanya kazi kwa karibu ili kufanikisha uchaguzi mkuu mwaka ujao. Wakati huo huo kiongozi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga amewaonya wanasiasa dhidi ya uhuni wa kiasiasa na semi za chuki akisema watakabiliwa na mkono wa sheria.