- 25,324 viewsDuration: 1:43BBC Verify imechambua video iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya Iran, inayoonyesha Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kikivamia meli mbili za mizigo katika Mlango wa Hormuz. Video hiyo inaonyesha boti ndogo zenye wanaume waliofunika sura zao na silaha wakikaribia meli za MSC Francesca na Epaminondas. Uchambuzi wa BBC Verify unaonyesha kuwa baadhi ya sehemu za video hiyo zinaonekana kurekodiwa saa kadhaa baada ya meli hizo kuripotiwa kutekwa na vikosi vya Iran. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw