Skip to main content
Skip to main content

Junior Starlets kukabiliana na Marekani katika Kombe la Dunia

  • | Citizen TV
    1,227 views
    Duration: 29s
    Timu ya taifa ya soka kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17, Junior Starlets, itamenyana na Marekani katika mchezo wake wa pili wa Kombe la Dunia usiku wa leo nchini Morocco. Junior Starlets wanahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kudumisha matumaini yao ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo, baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 3-0 dhidi ya China. Marekani kwa upande wake inalenga kuendeleza kiwango chake kizuri baada ya kuicharaza Samoa kwa mabao 17-0 katika mechi ya awali. Mechi hiyo itaanza saa tatu kamili usiku wa leo.