Skip to main content
Skip to main content

Kafyu yaathiri uchumi Lamu

  • | Citizen TV
    300 views
    Duration: 2:04
    Viongozi wa kidini na viongozi wa kijamii katika Kaunti ya Lamu wametoa wito kwa serikali ya kitaifa kuondoa amri ya kutotoka nje na vizuizi vingine vya muda mrefu vya usalama, wakisema vimelemaza uchumi wa eneo hilo na kukiuka haki za wakazi. Kulingana nao, licha ya kaunti ya Lamu kuwa na miundo musingi ya kuimarisha Uchumi wa taifa kama vile Barabara ya lami na Bandari kuu ya lamu katika mpango wa LAPSSET, amri iliyowekwa kwa takribani miaka 11 iliyopita ya kutotoka nje saa za usiku imeathiri uchukuzi na uwekezaji .