Skip to main content
Skip to main content

Kaunti 18 zaonywa kuhusu hatari ya mvua ya El Niño

  • | Citizen TV
    2,603 views
    Duration: 55s
    Taasisi ya Utabiri wa Hali ya Hewa imeorodhesha kaunti 18 zilizo katika hatari ya kuathiriwa na mvua ya El Niño. Kaunti za Pwani za Tana River, Kilifi, Lamu, Mombasa na Kwale zinatarajiwa kukumbwa na mafuriko pamoja na mawimbi makubwa ya baharini. Katika eneo la Nyanza, kaunti za Kisumu, Busia, Siaya, Homa Bay na Migori pia zinatarajiwa kukumbwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi. Katika eneo la Bonde la Ufa, kaunti za Turkana, Baringo, West Pokot na Narok ziko kwenye tahadhari kutokana na uwezekano wa mafuriko na athari nyingine za mvua kubwa. Kaunti za Garissa, Wajir na Mandera kaskazini mwa Kenya pia zimetajwa kuwa katika hatari, huku Idara ya Hali ya Hewa ikionya kuhusu uwezekano wa mafuriko jijini Nairobi.