- 6,657 viewsDuration: 2:55Serikali ya Kaunti ya Laikipia yapinga ujenzi wa Kituo cha Karantini ya ebola katika kaunti hiyo. Kwenye waraka wake mahakamani, waziri wa afya wa kaunti hiyo Albert Taiti asema kuwa mradi huo waibua wasiwasi mkubwa kuhusu afya ya umma kwa wakaazi wa eneo hilo. Taiti asema kuwa japo kaunti haipingi juhudi za kuzuia ugonjwa hatari wa ebola, ina hofu kuhusu namna mradi huo unavyotekelezwa.