- 3,951 viewsDuration: 56sMtu mmoja zaidi amethibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola nchini, na kufanya jumla ya maambukizi kufikia tisa. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, mgonjwa huyo alifanyiwa uchunguzi zaidi baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo. Mgonjwa huyo wa hivi punde ni mwanamume mwenye umri wa miaka 24, ambaye ni jamaa wa mgonjwa wa kwanza kuripotiwa nchini. Mgonjwa huyo wa kwanza alifariki hospitalini tarehe 5 Oktoba mwaka huu, siku chache baada ya kuwasili nchini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Jamaa huyo aliwekwa karantini. Aidha, watu 134 kati ya 135 waliokuwa wamewasiliana na mgonjwa wa kwanza wamefuatiliwa na kuwekwa karantini. Wizara ya Afya pia imesema imepokea dozi 500 za dawa za kuwasaidia wagonjwa waliotengwa.