Skip to main content
Skip to main content

Maafisa wa NACADA wafanya msako wa pombe haramu Kapsabet

  • | Citizen TV
    1,031 views
    Duration: 1:18
    Maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti Matumizi ya Dawa za Kulevya na Pombe (NACADA) wakishirikiana na maafisa wa usalama, wamefanya oparesheni kabambe mjini Kapsabet na kufanikiwa kunasa shehena kubwa ya pombe haramu. Maafisa hao walivamia chumba kimoja mjini humo ambapo walipata masanduku katoni 900 za pombe haramu zikiwa yzimehifadhiwa kwa siri. Washukiwa kadhaa walitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuuza na kusambaza vinywaji hivyo hatari huku gari moja likinaswa.