Skip to main content
Skip to main content

Mafuriko Tana River yaacha familia 3,000 bila makao

  • | Citizen TV
    888 views
    Duration: 3:00
    Zaidi ya familia 3,000 zinazoishi katika eneo la Talasa, kaunti ya Tana River, zimeachwa bila makao baada ya mafuriko kusomba nyumba zao. Mafuriko hayo yaliyosababishwa na Tana River kuvunja kingo zake yamewaacha wanafunzi kwenye njia panda huku wengi wakishindwa kuvuka mto huo kwenda shuleni. Mojawapo ya shule zilizoathirika zaidi ni Shule ya Msingi na Sekondari ya Odole yenye wanafunzi 700. Na kama anavyoarifu Serfine Achieng Ouma, Kenya Red Cross inasema kuwa wakazi hao ambao sasa wanaishi kwenye mahema wanahitaji msaada wa dharura wa chakula na bidhaa muhimu.