- 284 viewsDuration: 51sMashabiki wa kipindi cha Kutubuti kwenye kituo cha Bahari FM kinachodhaminiwa na Royal Media Services walikongamana mjini Mombasa kwa mashindano ya kila mwaka ya Kutubuti Cup. Mashabiki wa timu ya Arsenal walinyakuwa ubingwa kwenye mchuano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Serani Mombasa. Mashabiki wa kituo hicho hukongamana kila mwaka kusherehekea kipindi cha michezo chenye ufuasi mkubwa Pwani.