Maafisa wakuu serikalini, wakiwemo makatibu-9, wanakabiliwa na uchunguzi kuhusiana na marupurupu na malipo mengine wanayodaiwa kulipwa kuhusiana na mpango wa Huduma Kenya. Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Nancy Gathungu ameelezea wasiwasi wake kuhusu uhalali wa usimamizi wa mpango wa Huduma Kenya, unaodaiwa kuhudumu kwa miaka 13 iliyopita bila sera kamili au mipangilio ya kisheria, ingawa maafisa hao wameendelea kupokea marupurupu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive