Skip to main content
Skip to main content

Msichana adai kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya mafuta

  • | Citizen TV
    5,164 views
    Duration: 2:53
    Msichana mwenye umri wa miaka 19 anaitaka Idara ya Polisi kuwajibika baada ya kudaiwa kupigwa risasi na afisa wa polisi wakati wa maandamano ya kupinga nyongeza ya bei ya mafuta. Sharon Nyambura anasema alipigwa risasi akiwa mtaani Kahawa West alipokuwa akisukwa nywele, wakati maandamano hayo yakiendelea katika eneo hilo. Sasa anadai haki na uwajibikaji kutoka kwa mamlaka husika, akisema tukio hilo limebadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa. Franklin Wallah ana taarifa zaidi.